Skip to main content

Wakati umefika kwa kila Mtanzania kushirikiana kwa dhati kuhakikisha hakuna anayenyimwa haki yake kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali au uelewa wa kisheria

Submitted by admin on 30 December 2024

Msaada wa kisheria ni haki ya msingi ambayo inalenga kuhakikisha kila raia wa Tanzania anapata fursa ya kutetea haki zake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria mbalimbali zilizopo. Katiba ya Tanzania, hususan Ibara ya 13(6)(a), inatamka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kusikilizwa kwa usawa mbele ya vyombo vya kisheria bila ubaguzi wowote.

Hata hivyo, changamoto kama umasikini, ukosefu wa elimu ya kisheria, na umbali wa huduma za kisheria zimewafanya baadhi ya wananchi kushindwa kufikia haki zao ipasavyo. 

Hili limeifanya serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kuanzisha juhudi za kuimarisha msaada wa kisheria kupitia kampeni Ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Msaada wa kisheria si huduma ya hiari bali ni haki kwa kila raia wa Tanzania. 

#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango @biteko

@katibanasheria_ @profkabudipjam @Victoriamwanziva @tanganyikalawsociety @boniface_a_k_mwabukusi