Wanawake wa jamii za kifugaji wameelezea shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaletea elimu na msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (MSLAC). Kupitia kampeni hii, wamama wa kifugaji wamepata uelewa kuhusu haki zao katika masuala ya ardhi, ndoa, mirathi, na ulinzi wa watoto, huku wakihamasishwa kutumia njia mbadala za utatuzi wa migogoro kama usuluhishi na maridhiano.
Katika video hii, tunashuhudia mafanikio ya msaada huu wa kisheria, simulizi za wanufaika, na namna elimu hii inavyobadilisha maisha ya wanawake wa jamii za kifugaji kwa kuwapa sauti na ujasiri wa kutetea haki zao.
📌 Tazama, Like, Comment, na Subscribe kwa habari zaidi kuhusu haki na msaada wa kisheria!
#SamiaLegalAid #MSLAC #HakiKwaWote #MamaSamia #WanawakeKifugaji #MsaadaWaKisheria