Skip to main content

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Kilwa wamenufaika na elimu ya ukatili wa kijinsia pamoja na sheria mbalimbali zinazohusiana na masuala hayo.

Submitted by admin on 20 March 2025

Image

Elimu hiyo ilitolewa na wataalamu wa masuala ya kijinsia na wanasheria waliolenga kuwaelimisha wanafunzi kuhusu aina za ukatili wa kijinsia, athari zake, na njia za kuzuia vitendo hivyo Pia, walitoa ufafanuzi wa sheria mbalimbali zinazolinda haki za binadamu, hasa haki za watoto na vijana, na kuhimiza wanafunzi kuripoti vitendo vya ukatili vinapojitokeza

Image

Lengo kuu la programu hiyo ni kuwajengea wanafunzi ufahamu wa haki zao, kuwasaidia kujitambua, na kuwawezesha kushiriki katika kuimarisha jamii yenye usawa na haki. Aidha, viongozi wa shule hiyo walieleza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa wanafunzi wao kwani inawasaidia kuwa raia wema wanaoheshimu na kulinda haki za wenzao

Image

Shule ya Sekondari ya Kiislamu Kilwa imejipanga kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha elimu ya masuala ya kijinsia inatolewa kwa wanafunzi kwa kina ili kujenga kizazi chenye ufahamu bora wa masuala ya kijamii.

@samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa

@hakingowinews @katibanasheria_ #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya