Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) imeendelea kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wa Kata ya Buhendangabo, wilayani Bukoba, mkoani Kagera. Elimu hii inalenga kuwawezesha wananchi kuelewa haki zao kisheria katika masuala ya ardhi, mirathi, ndoa, ajira, na ukatili wa kijinsia. Pia, wananchi wamehamasishwa kutumia njia mbadala za kutatua migogoro kama upatanishi, usuluhishi, na mashauriano ya amani. Kampeni hii inalenga kujenga jamii yenye haki na utulivu wa kijamii kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata mwongozo wa kisheria unaofaa.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano