Arusha, Machi 1 – 3,Katika siku ya tatu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wanasheria wamejitokeza na kutoa ushuhuda wa mafanikio makubwa katika utatuzi wa migogoro ya wananchi, wakionesha jinsi huduma za kisheria zinavyoweza kuleta suluhisho la haki na amani.
Miongoni mwa wanasheria waliotoa ushuhuda ni wale waliotoa msaada wa kisheria kwa wanawake waliokumbwa na changamoto za mirathi, ndoa, na haki za mali, ambapo walisema kuwa njia mbadala za utatuzi wa migogoro (ADR) zimechangia kupunguza mzigo wa kesi mahakamani na kuimarisha mahusiano ya kijamii.
Wakili Baraka Elias Sulus, alieleza jinsi usuluhishi wa migogoro ya ardhi ulivyosaidia familia nyingi kuepuka migogoro ya muda mrefu, akisema: “Tunapowasaidia wananchi kupata haki zao kwa njia za amani, tunajenga jamii yenye mshikamano na maendeleo endelevu.”
Wananchi waliopata msaada wa kisheria pia walitoa ushuhuda wao, wakieleza namna walivyonufaika na usaidizi wa kitaalamu, huku wakihamasisha wengine kutumia huduma hizo kwa ajili ya haki na ustawi wa jamii.
Maadhimisho haya yanaendelea kushamiri kwa mijadala na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao, hasa kwa wanawake, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha usawa wa kijinsia na upatikanaji wa haki kwa wote. ANGALIA VIDEO KWENYE COMENTS