FAMILIA ya watoto saba wenye umri chini ya miaka 10 wamekuwa wakijitunza wenye kwa muda wa miaka mitatu kutokana na wazazi wao wakutengana .
Watoto hao wameibuliwa na kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inayoendelea wilayani hapa hapa baada ya kuzinduliwa januari 10 mwaka huu.
Timu ya wanahabari wa Mama Samia Legal Aid Campaign iilifanikiwa kuongea na mmoja wa watoto hao walipofika makao makuu ya wilaya ya Ikungi kukutana na timu ya kampeni hiyo iliyowaita baba mama na watoto hao wote ili kupata chanzo ya tattoo hilo .
Akizungumza tukio hilo mmoa wa watoto wa familia hiyo (jina linahifadhiwa) alisema wamekuwa wakijitunza kwa muda wote huo kutokana na wazazi wao kutengana na mama yao alikwenda kuishi nyumbani kwao.
Alibainisha kuwa wanakaa na baba yao anayeitwa Temistocules Ijengo na amekuwa hawahudumiaa kutokana na kushinda muda mwingi kwenye pombe hivyo hajui watoto hao kuwa wamekula nini.
Aliongeza kwa sasa anasoma shule ya msingi lakini amekuwa haudhurii masomo vizuri kutokana na kutumia muda mwingi kuwahudumia wenzake kwa kuomba omba chakula kwa watu ili kuwatunza wenzake.
Alisema mama yake aliondoka na kuwaacha watoto hao sita huku akimwacha mmoja wa watoto hao akiwa mdogo mwenye umri wa chini ya miaka miwili na alimtunza mpaka sasa ana umri wa miaka minne.
Pia alisema wakizidiwa na hali ya njaa wamekuwa wakienda kwa mama yao kuomba msaada wa chakula ili kujitunza na wamekuwa na tabia ya kumbakishia baba yao chakula kikipatikana kwa kuwa wanampenda na wasingependa kuona anakufa kwa njaa.
Kiongozi wa timu ya kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria Wilaya ya Ikungi, Laurent Burilo akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo jana alisema kuwa wakiwa katika Kijiji cha Mwis wilayani hapo kwa ajli ya kutoa elimu ya msada wa kisheria walipata taarifa ya watoto kupitia viongozi wa Kijiji hicho.

Burilo alisema baada ya taarifa hizo walichukua jukumu la kuanza kuwatafuta wazazi hao na walifanikiwa mwisho wa wiki kukutana nao na kufanya mazungumzo kwa wote wawili yaani Mke na mume.
Kadhalika alisema kuwa walianza kwanza kufanya mazungumzo na mmoja mmoja na kuwaeleza madhara ya maisha ya watoto wao na ndipo walipowakutanisha wote na kufanikiwa kuwaunganisha tena familia hiyo pamoja na watoto wao ambao nao walifika katika neo hilo.
Mmoja wa majirani wa familia hiyo Emanuel Ntandu ambaye naye alishiriki kuwasafirisha watoto hao pamoja na baba yao kutuka Kijijini kuwafikisha eneo hilo la makao makuu wa wilaya alisema wamekuwa wakiwasaidia chakula watoto hao mara kwa mara na wamekuwa wakilalamikia tatizo hilo kwa muda.
Aliishukuru kampeni hiyo ya mama Samia kwa kufika hapo na kuwasaidia watoto hao na ambao wameishi kwa shida wa muda huo wa miaka mitatu.
Mama wa watoto hao Neema Joseph akizungumza na waandishi wa habari alisema aliikimbia ndoa yake kutokana na unyanyasaji kutoka kwa mume wake Temistocules Ijengo.
Neema alisema siku ya mwisho kuondoka kwake hapo alishuhudia mume wake akiwapiga watoto na alipohoji naye alipigwa sana akaona bora aokoe uhai wake.
Afisa Ustawi Wilaya ya Ikungi ,Beatrice Maeda alisema baada ya kufanikiwa kuwaunganisha tena familia hiyo wataendelea kuifuatilia na Temistocules atakuwa akiripotia ofisi ya Mtendaji wa Kijiji kila siku kwa muda wa mwezi moja kuangalia mwenendo wake na taarifa hizi zitakuwa zikifikishwa kituo cha polisi kila siku.
Maeda endapo akikiuka masharti hayo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa sababu ndiye aliyeonekana kusababisha familia hiyo kutengana.
- Log in to post comments