Katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Tanga, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amekutana ana kwa ana na wananchi na kusikiliza migogoro mizito inayowakabili.
Migogoro hiyo ilihusu maeneo ya ardhi, ndoa, mirathi, haki za wanawake na watoto, pamoja na kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu. Waziri Ndumbaro amesisitiza kuwa serikali ipo tayari kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki kwa wakati, kwa njia rafiki na bila gharama kupitia huduma za msaada wa kisheria.
Mhe. Ndumbaro pia amesisitiza dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusogeza haki karibu na wananchi kupitia kampeni hii ya kitaifa.
📍 Tazama video hii ujionee namna serikali inavyoshughulikia kwa vitendo changamoto za kisheria zinazowakabili wananchi.
🔔 Subscribe kwa elimu zaidi kuhusu haki zako na taarifa muhimu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria. #DamasNdumbaro #MoCLA #MsaadaWaKisheria #MamaSamia #UzinduziTanga #HakiKwaWote #LegalAidTanzania #KatibaNaSheria #Tanzania2025