Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kutekeleza falsafa ya '4R' iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maboresho ya masuala mbalimbali kwenye taasisi zote zilizopo chini yake.