Skip to main content

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAANZISHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA - BW. OMARY, MKURUGENZI WA TEHAMA.

Submitted by admin on 21 August 2025

Wizara ya Katiba na Sheria imezindua Kituo cha Huduma kwa Mteja ili kurahisisha mawasiliano kati ya wananchi na wizara. Hatua hii inalenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma za kisheria kwa wote.

Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Omary Gabriel, amesema kituo hiki kitasaidia wananchi:

✅ Kupata taarifa sahihi kwa haraka

✅ Kuwasilisha maoni na malalamiko kidijitali

✅ Kupunguza usumbufu wa kufuata huduma makao makuu

💡 Huduma hii ni sehemu ya mageuzi ya kidijitali serikalini, ikionyesha dhamira ya serikali kuimarisha upatikanaji wa haki na kuwa karibu zaidi na wananchi.

👉 Tazama video hii ufahamu faida na umuhimu wa Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa jamii ya Watanzania.

#KatibaNaSheria #HudumaKwaMteja #Tanzania