Arusha, Machi 1, 2025 – Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maximilian, ametangaza kuwa zaidi ya watu laki nne wanatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhe. Maximilian amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika, huku serikali ya jiji na wadau mbalimbali wakihakikisha hafla hiyo inafanikiwa kwa kiwango cha juu. "Tunaendelea kuhakikisha kuwa miundombinu yote muhimu iko tayari ili wageni kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi waweze kushiriki kwa amani na utulivu," alisema.
Ameongeza kuwa maadhimisho haya yataambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala kuhusu haki za wanawake, usawa wa kijinsia, na maendeleo ya kiuchumi kwa wanawake. Aidha, kutakuwa na maonyesho ya bidhaa na huduma zinazotolewa na wanawake wajasiriamali, pamoja na burudani za kitamaduni kutoka vikundi mbalimbali vya sanaa.
#sisinitanzania #mslac #katibanasheria #kaziiendelee #ssh #ccm #matokeochanya #nchiyangukwanza #habari #news