Katika zoezi lililofanyika hivi karibuni, mwananchi mmoja kutoka kijiji cha Kisiju aliwasilisha kesi ya mgogoro wa ardhi ambayo ilihitaji ufafanuzi wa kisheria. Afisa huyo alimsikiliza kwa makini na kutoa maelezo ya kina kuhusu sheria za ardhi na namna ya kushughulikia mgogoro huo kwa njia ya amani kupitia mbinu za usuluhishi na maridhiano.
Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Maendeleo, lengo kuu la Dawati la Msaada wa Kisheria ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kisheria na huduma stahiki ambazo zitawawezesha kulinda haki zao bila kuingia gharama kubwa za kisheria. "Tunahakikisha tunatoa msaada wa kisheria ili kupunguza changamoto za migogoro isiyoisha. Hii ni njia ya kujenga jamii yenye utulivu na mshikamano," alisema afisa huyo.
Wananchi waliohudhuria zoezi hilo walieleza kufurahishwa kwao na msaada walioupata. "Kwa mara ya kwanza nimeelewa sheria za ardhi na hatua za kuchukua ili kutatua matatizo bila ugomvi. Nawashukuru sana kwa elimu hii," alisema mmoja wa wanakijiji.
Dawati la Msaada wa Kisheria katika Wilaya ya Mkuranga limekuwa likitoa msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali ikiwemo ndoa, urithi, migogoro ya ardhi, unyanyasaji wa kijinsia, ajira, na kesi za jinai. Mpango huu ni sehemu ya juhudi za serikali na wadau wake kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata fursa ya kuishi kwa amani na kufuata sheria.
Kwa kupitia kampeni kama hii, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, hasa wale walioko pembezoni. Wananchi wanahimizwa kuendelea kufika katika Dawati la Msaada wa Kisheria ili kupata huduma hizi muhimu, huku wakikumbushwa umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan Ikulu Mawasiliano Ikulu Mawasiliano