Skip to main content

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, siku ya Jumatano, alitoa huduma kwa mama mjane mwenye watoto watatu, ambaye amekuwa akinyanyaswa na shemeji yake tangu kufariki kwa mume wake mwaka 2017

Submitted by admin on 21 December 2024

Mama huyo ameporwa shamba na nyumba, hali ambayo imezidi kumuweka katika mazingira magumu ya maisha. 

Afisa huyo alifika kutoa usaidizi wa kisheria na kijamii, akilenga kuhakikisha haki ya mama huyo inalindwa na kwamba anapata mali zake alizonyang’anywa kinyume na sheria. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kusaidia makundi yaliyo hatarini na kuhakikisha ustawi wa familia zinazoishi katika changamoto kama hizi. #MSLAC. #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @IkuluMawasiliano