Skip to main content

BIB NA SAFARI YA MIAKA 20 KUTAFUTA HAKI, MSLAC YAMPATIA SULUHU CHANYA NA KUPATA HAKI YAKE.

Submitted by admin on 8 March 2025

Safari ya muda mrefu hatimaye yafikia ukomo, haki ya Bibi yakamilika kupitia msaada wa MSLAC

Kwa zaidi ya miaka 20, Bibi mmoja amekuwa akisaka haki yake bila mafanikio, akisumbuka katika vyombo vya sheria na jamii kwa jumla. Safari yake ya kudai haki iligubikwa na changamoto lukuki, zikiwemo ucheleweshaji wa maamuzi, ukosefu wa msaada wa kisheria, na changamoto za kifamilia zilizozuia kupatikana kwa suluhu ya haki yake.

Hata hivyo, kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (MSLAC), matumaini yake yalirejea tena. Kupitia msaada wa wataalamu wa sheria wa MSLAC, suala lake lilifanyiwa uchambuzi wa kina, hatua stahiki zikachukuliwa, na hatimaye alifanikiwa kupata haki yake.

#mslac #katibanasheria #sisinitanzania #ssh #matokeochanya #nchiyangukwanza #ccm #hakikwawote #habari