MAMA SAMIA LEGAL LEGAL AID YAMPATIA MWANAIDI HAKI YA ARDHI ILIYOTOLEWA KWA SHULE Katika kampeni maalumu ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayoendelea katika Uwanja wa TBA jijini Arusha, Mwanaidi Mussa Hussein ameonesha furaha kubwa baada ya kupata haki yake ya ardhi aliyoikosa zaidi ya miongo miwili.
Mwanaidi anasimulia kuwa tangu mwaka 1997 alikuwa akimiliki ardhi baada ya kifo cha mume wake, ardhi ambayo ilichukuliwa na Ofisi ya Ardhi kwa ajili ya upanuzi wa Shule ya Msingi Unga Limited, ikimuahidi kumpa ardhi mbadala, lakini, alikumbana na ucheleweshaji wa kupata ardhi hiyo.
Baada ya kusikia habari kuhusu Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Mwanaidi aliamua kuchukua hatua kwa kuanza kufuatilia haki yake, hatimaye kupitia kampeni hiyo ameipata, na tayari ameshapokea hati ya kiwanja mbadala kilichopo eneo la Oljoro.
Kwa maneno ya Mwanaidi, kampeni hii ni ishara ya juhudi za serikali katika kuhakikisha haki za wananchi zinatolewa haraka na kwa ufanisi, na ni mfano wa jinsi huduma za kisheria zinavyoweza kuboresha maisha ya watu ambao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya muda mrefu.