Inaweka wazi kuwa kila Mtanzania ana stahiki ya kupata haki bila ubaguzi. Haki hizo si zawadi ya mtu binafsi wala taasisi, bali ni wajibu wa kikatiba na kisheria kwa kila raia kuzipata na kulindwa nazo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndiye mlezi mkuu wa kampeni hii. Kupitia uongozi wake, Serikali imehakikisha huduma za msaada wa kisheria zinapatikana bure kwa wananchi hasa wale wa kipato cha chini, ili kuhakikisha hakuna anayekosa haki kwa sababu ya ukosefu wa fedha au uelewa mdogo wa sheria.
#WizaraYaKatibaNaSheria #HudumaKwaWananchi #MamaSamiaLegalAid #HakiKwaWote #HakiSawa #MsaadaWaKisheria #SheriaNiNguvu #ElimuYaSheria #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #TanzaniaNiwajibuwetu #Nchiyetufahariyetu #tanzania #SSH