Siku hii muhimu imekuwa fursa ya kuwakutanisha wanawake kutoka maeneo mbalimbali, kuadhimisha mafanikio yao, na kujadili changamoto zinazowakabili.
Maadhimisho haya hayakuwa tu sherehe, bali pia yalikuwa jukwaa la elimu na uwezeshaji. Wataalamu wa Msaada wa Kisheria wa Mama samia legal aid (MSLAC) walishiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wanawake. Elimu hii ililenga kuwajengea uwezo wanawake katika kufahamu haki zao na kuzitetea.
Wataalamu wa MSLAC walitoa ufafanuzi wa kina kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria yanayowahusu wanawake, ikiwa ni pamoja na: * Ukatili wa kijinsia * Haki za ardhi * Mirathi * Talaka na malezi ya watoto
Mbali na elimu ya kisheria, wataalamu wa MSLAC pia walishughulikia changamoto mbalimbali zilizowakabili wanawake.
#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #MatokeoChanya