Skip to main content

HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA YAENDELEA KILIMANJARO KUPITIA KAMPENI YA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

Submitted by admin on 7 February 2025

Image

Huduma ya msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) inaendelea katika Halmashauri ya Hai, mkoani Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi. Wananchi wanapewa mwongozo juu ya masuala ya ardhi, ndoa, mirathi, mikataba ya ajira, na ukatili wa kijinsia. Aidha, wananchi wamehamasishwa kuandika wosia na kutatua migogoro kupitia njia mbadala kama upatanishi na usuluhishi. Kampeni hii inalenga kujenga jamii inayojitambua kisheria na yenye utulivu wa kijamii.

#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango @DBiteko

@katibanasheria_ @profkabudipjam @victoriacharlz @tanganyikalawsociety @BMWABUKU