Kupitia kampeni hii, wananchi wanapatiwa msaada wa kisheria bure unaolenga kuwasaidia kutatua migogoro ya ardhi kwa njia ya haki na kikatiba. Hii inafanyika kwa kutoa elimu ya kisheria, kusaidia wananchi kuelewa haki zao za kikatiba, na kuwasaidia kufuata taratibu sahihi za kisheria ili kuepuka migogoro.