Skip to main content

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI FURSA KUU KWA WATANZANIA NA MFANO WA KUIGWA AFRIKA. PASTOR GEORGE

Submitted by admin on 13 March 2025

Pastor George kutoka Cameroon amepongeza juhudi za Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, katika kuanzisha na kuendeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria (MSLAC). Akitilia mkazo umuhimu wa mpango huu, Pastor George amesema kuwa kampeni hii ni fursa adhimu kwa Watanzania, hasa wale wa kipato cha chini, kupata elimu ya kisheria na msaada wa bure katika kutatua migogoro inayowakabili, hususan katika masuala ya ardhi, ndoa, mirathi, na haki za binadamu.

Pastor George ameainisha kuwa, katika mataifa mengi ya Afrika, wananchi wengi wanakosa uelewa wa kisheria na kushindwa kupata haki zao kwa sababu ya gharama kubwa za huduma za sheria. Ameeleza kuwa mfano wa Tanzania kupitia uongozi wa Mama Samia unapaswa kuigwa na mataifa mengine ya Afrika, kwani unawapa wananchi fursa ya kujua haki zao na kujenga jamii yenye usawa na haki.

#mslac #sisinitanzania #katibanasheria #matokeochanya #nchiyangukwanza #ssh #ccm #hakikwawote #kaziiendelee #habari