Kauli mbiu hii inaashiria azma ya Mhe. Rais ya kulinda, kukuza na kutetea Haki za Wananchi wanyonge na kupinga vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu, misingi ya utawala bora, ukatili wa kijinsia na kuheshimu utawala bora na utawala wa Sheria ambayo ni msingi wa maendeleo ya Nchi. Kampeni hii inatekeleza falsafa ya 4R ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo ni maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resiliance), Mageuzi (Reforms) na kujenga upya Taifa (Rebuilding) kwani bila misingi imara ya utawala wa sheria na utoaji haki ambayo ni majukumu ya muhimu ya Wizara ya Katiba na Sheria ni vigumu kutekeleza falsafa hii.