Skip to main content

MAANDALIZI UJIO WA MSLAC MKOANI KAGERA

Submitted by admin on 12 April 2025

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Stephen Mashauri Ndaki akiongoza kikao cha maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia (MSLAC) mkoani Kagera uzinduzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 14  Aprili, 2025 katika viwanja vya Jamhuri (Mashujaa) mkoani humo.

Image

Image

Image

Kikao hicho kimehudhuriwa na  wataalam kutoka  Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria wa Wizara Ester Msambazi pamoja na  wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ikiwa ni sehemu ya kupeana majukumu na kubadilisha uzoefu ili kufanikisha hafla  ya  uzinduzi na utekelezaji  wa Kampeni mkoani Kagera.