MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Siku ya Wanawake Duniani imeadhimishwa kwa hamasa kubwa jijini Arusha, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza dhamira ya serikali kujenga jamii jumuishi, yenye haki na usawa wa kijinsia.
Maadhimisho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, yakihudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sekta mbalimbali za uchumi.
Rais Dkt. Samia ameeleza hatua muhimu ambazo Tanzania imepiga katika kufanikisha malengo ya
Azimio la Beijing la 1995 na Dira ya Maendeleo Endelevu.
Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kupambana na mila kandamizi na kuhakikisha kila msichana na mwanamke anapata fursa sawa kufanikisha ndoto zake.
Aidha, alihimiza uwekezaji kwa vijana ili kuimarisha harakati za usawa wa kijinsia kwa vizazi vijavyo.
Maadhimisho haya yamekuwa jukwaa muhimu la tathmini na kuweka mikakati yakuendeleza haki za wanawake nchini.