Arusha, Machi 3, 2025 – Katika jitihada za kusaidia wananchi kupata haki zao, kampeni ya msaada wa kisheria imeendelea kuwafikia watu mbalimbali nchini, huku Yahya Muhamed Marsha, mkazi wa Arusha, akieleza matumaini yake makubwa kwa huduma hii.
Akizungumza mara baada ya kupokea ushauri wa kisheria, Yahya alisema, "Matumaini yangu yote yapo kwenye huduma hii ya kisheria, naona hapa nimefika na nitasaidika kisheria." Kauli yake inaonesha jinsi huduma za msaada wa kisheria zinavyokuwa mwanga kwa wananchi wanaopitia changamoto za kisheria lakini hawana uwezo wa kupata mawakili binafsi.
Kampeni hii imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria, hasa wale wanaokabiliwa na changamoto za migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, ajira, na masuala mengine ya kisheria. Wadau wa sheria wameendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kupata elimu na msaada wa kisheria ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote.
Huduma hizi zinaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali, huku wito ukiendelea kutolewa kwa serikali na mashirika binafsi kuunga mkono juhudi hizi ili kuzidi kuwafikia wananchi wengi zaidi.
#mslac #sisinitanzania #katibanasheria #ssh #ccm #matokeochanya #nchiyangukwanza #habari #news