Skip to main content

MHE: AMONI MPANJU ATOA SALAMU ZA WIZARA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA ARUSHA.

Submitted by admin on 29 March 2025

Mhe. Amoni Mpanju, Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, anatoa salaam za Wizara katika uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia uliofanyika mkoani Arusha tarehe 28 Machi 2025.

Katika hotuba yake, Mhe. Mpanju amepongeza jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha upatikanaji wa haki kwa Watanzania wote, hususan wanawake, watoto, wazee, na makundi maalum. Amesisitiza umuhimu wa elimu ya sheria kwa wananchi ili kuondoa migogoro na kuongeza amani katika jamii.

🟢 Kampeni hii inalenga:

Kuwafikia wananchi wa kada zote na kuwaelimisha kuhusu haki zao za kisheria

Kutoa msaada wa kisheria bure kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili

Kukuza utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kama usuluhishi na maridhiano

👥 Imeandaliwa na:Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Kitengo cha Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Sheria.

📢 Tazama, Sikiliza, na Shiriki ujumbe huu wa kuhamasisha haki kwa wote!

#MSLAC #MamaSamia #MsaadaWaKisheria #HakiKwaWote #Tanzania #MaendeleoYaJamii #Arusha