Tanzania inaendelea kuthibitisha kuwa ni kinara wa haki na usawa kwa wote, bila kujali uraia au asili. Raia wa Cameroon, PASTOR GEORGE ACHO, ambaye alikutana na changamoto za kisheria nchini, ameweza kupata msaada wa kisheria kwa haraka na bila vikwazo kupitia mpango wa Samia Legal Aid Campaign (MSLAC).
Akizungumza baada ya kupatiwa msaada huo, Mkameruni huyo aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mifumo madhubuti inayowezesha watu wote, wakiwemo wageni, kupata haki zao kwa urahisi.
"Tanzania imenifundisha kuwa haki haichagui uraia! Huduma ya msaada wa kisheria hapa ni ya kiwango cha juu, na ninamshukuru sana Rais Samia kwa kuhakikisha mfumo huu unafanya kazi bila ubaguzi," alisema kwa furaha. -- PASTOR GEORGE ACHO
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kusimamia upatikanaji wa haki kwa wote, huku mpango wa MSLAC ukizidi kuwafikia wananchi wa makundi yote, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Rais Samia ya kujenga jamii yenye haki na usawa
Hatua hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika katika masuala ya utawala wa sheria na upatikanaji wa haki kwa wote. #HakiKwaWote 🇹🇿⚖️
#SamiaLegalAid #TanzaniaYaHaki #mslac #sisinitanzania #katibanasheria #matokeochanya #ccm #nchiyangukwanza #kaziiendelee #hakikwawote #habari