Skip to main content

MSAADA WA KISHERIA MKOANI KIGOMA: KUIMARISHA HAKI NA USAWA KWA WANANCHI

Submitted by admin on 24 January 2025

Mkoa wa Kigoma umeendelea kunufaika na huduma za msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Samia Legal Aid Campaign (MSLAC), ambayo inalenga kutoa elimu ya kisheria na kuhakikisha haki za wananchi zinazingatiwa. Msaada huu wa kisheria unalenga makundi mbalimbali ya jamii, yakiwemo wakulima, wavuvi, wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu ambao mara nyingi wanakabiliwa na changamoto za kisheria kutokana na ukosefu wa elimu na rasilimali.

Image

Image