Waziri wa Katiba na Sheria, akiongozana na timu ya wanasheria, ameendelea na juhudi za kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa Kibilizi, Kigoma kupitia kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (MSLAC).
Elimu imetolewa kuhusu masuala ya ardhi, ndoa, mirathi, ajira, na ukatili wa kijinsia. Wananchi wametakiwa kutumia fursa hii ya kipekee kuboresha uelewa wa haki zao za kisheria na kutatua migogoro kwa njia za amani. Kampeni hii inaendelea kuleta mabadiliko makubwa kwa jamii.