Skip to main content

MSLAC NDANI YA KARATU

Submitted by admin on 4 April 2025

Wataalamu wa msaada wa kisheria kutoka Mama Samia Legal Aid wametoa elimu kuhusu huduma za msaada wa kisheria na mfumo wa MSLAC kwa wananchi wa Kata ya Baray, Kijiji cha Matala, ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.

Image

Image

Lengo la zoezi hili lilikuwa kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao za kisheria, taratibu za kupata msaada wa kisheria, na namna MSLAC inavyoweza kusaidia katika kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote, hususan makundi yenye uhitaji maalum kama wanawake, watoto, na wazee.

Image

#Katibanasheria #MSLAC #sisinitanzania #Hakikwawote #Nchiyangukwanza #kaziendelee