Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wakitoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kupitia Kampeni ya Huduma za Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) katika shule ya Msingi Sanze iliyopo kata ya Kisarawe. Wanafunzi wameelimishwa kuhusu Matunzo ya watoto, Haki za watoto, Haki za Binadamu kwa Ujumla, Sheria ya Ndoa, Haki za Mirathi kwa Watoto, Namna ya kuweza kuepuka, kujilinda, na kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili wa Kijinsia na Usuluhishi wa Migogoro mbalimbali kwa njia mbadala.
#SSH #kaziiendelee #sisiniTanzania #MSLAC #matokeochanya #Kisarawedc