Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (MSLAC) imejizatiti kupambana na changamoto na migogoro inayowakumba kina mama nchini, ikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa, urithi, na ukatili wa kijinsia. Kupitia utoaji wa elimu ya kisheria na njia mbadala za utatuzi wa migogoro kama usuluhishi na maridhiano, MSLAC inalenga kuhakikisha wanawake wanapata haki zao kwa haraka na ufanisi.