Katika jitihada za kuimarisha upatikanaji wa haki na amani kwa jamii, timu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii (CDOs) ikishirikiana na Baraza la Kata la Migogoro la Mpandandogo, Halmashauri ya Tanganyika, ilifika katika eneo la shamba lililokuwa na mgogoro wa mipaka.
Ziara hiyo, iliyoendeshwa chini ya mwavuli wa Kampeni ya Samia Legal Aid Campaign (MSLAC), ililenga kusikiliza pande zote zinazohusika na kufanikisha mazungumzo ya amani. Timu ilihimiza majadiliano ya wazi, kusikilizana, na kufikia makubaliano ambayo yangeridhisha pande zote.
Baada ya majadiliano ya kina na ya haki, suluhu ilipatikana kwa kuridhisha, na pande zote mbili zilikubaliana kurejea kwa amani katika maisha yao ya kila siku. Hii ni ishara ya umuhimu wa msaada wa kisheria katika kutatua changamoto zinazowakumba wananchi katika maeneo yao.
Kauli mbiu ya MSLAC, "Msaada wa Kisheria ni Popote na kwa Hali Yoyote," ilidhihirishwa kwa vitendo kupitia tukio hili. Wananchi walipongeza juhudi za timu ya MSLAC na Baraza la Kata kwa kuhakikisha haki na amani vinatawala.
MSLAC inaendelea kuonyesha kuwa msaada wa kisheria siyo ndoto tena, bali ni haki halisi inayoweza kupatikana popote na kwa mtu yeyote, bila kujali changamoto zilizopo.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango