Maana ya ujumbe huu: Sheria haikutungwa kwa ajili ya kundi dogo la watu au wenye nafasi fulani pekee, bali ipo kwa ajili ya wananchi wote bila ubaguzi.
Kila raia ana haki ya kulindwa na sheria na pia wajibu wa kuifuata.
Hakuna mtu aliye juu ya sheria; wote ni sawa mbele ya sheria.
Ujumbe huu unahamasisha wananchi kutambua kuwa wanapohitaji msaada wa kisheria, si upendeleo bali ni stahiki yao kwa mujibu wa sheria.
Kupitia kampeni hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zinapatikana bure kwa wananchi wote, hususan wale wa kipato cha chini, ili kutekeleza dhana ya sheria kwa wote na si wachache.
#WizaraYaKatibaNaSheria #HudumaKwaWananchi #MamaSamiaLegalAid #SSH #kazinaututunasongambele #matokeochanya #SioNdotoTena #HakiKwaWote #HakiSawa #MsaadaWaKisheria #SheriaNiNguvu #ElimuYaSheria #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #TanzaniaNiwajibuwetu #Nchiyetufahariyetu #tanzania