Skip to main content

"SIO VIJANA MASHALOBARO TU, HADI WATU WAZIMA WANAINGIA KWENYE USHETANI" MKUU WA MKOA TANGA

Submitted by admin on 7 April 2025

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, leo tarehe 07 Machi 2025 ameongoza kikao cha maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho tarehe 08 Machi 2025.

Katika kikao hicho, Mhe. Dkt. Burian ameelezea namna vijana na watu wazima wanavyoshiriki katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na changamoto nyingine zinazohitaji msaada wa kisheria.

Kampeni hii ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na kwa usawa.

🔔 Subscribe ili kufuatilia matukio yote muhimu na elimu ya kisheria kutoka mkoani Tanga na maeneo mengine nchini.

#Tanga #MamaSamia #MsaadaWaKisheria #UnyanyasajiWaKijinsia #RCBatildaBurian #HakiKwaWote #LegalAid #ElimuYaKisheria