Skip to main content

SOPHIA RAMADHAN APATA MSAADA WA KISHERIA KUTOKA KWA WAZIRI NDUMBARO KUHUSU MDAI YA MIRATHI

Submitted by admin on 9 April 2025

Katika mwendelezo wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Tanga, Sophia Ramadhan Msikiti aliibua madai ya mirathi mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Sophia, ambaye alikuwa mke wa pili wa marehemu, alieleza jinsi shemeji yake anavyotaka kuuza nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu, licha ya kuwa ni sehemu ya urithi wake.

Kutokana na hali hiyo, Sophia aliamua kufungua kesi mahakamani kutafuta haki yake. Baada ya kusikiliza kwa makini, Mhe. Ndumbaro aliamuru apewe mwanasheria maalum wa serikali ili amwakilishe na kumsimamia katika kesi hiyo ya mirathi.

Tukio hili linaonyesha kwa dhahiri dhamira ya dhati ya serikali kupitia kampeni hii kuhakikisha wananchi wote, hasa wanawake, wanapata haki zao kwa njia ya kisheria.

#MsaadaWaKisheria #MamaSamia #SophiaRamadhan #Mirathi #WaziriNdumbaro #HakiKwaWote #Tanga