Skip to main content

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA INAYOHUSIKA NA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NASHERIA

Submitted by admin on 4 December 2024

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi leo tarehe 04 Desemba, 2024 amekutana na kufanya kikao na  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Imani Aboud aliyeambatana  na ujumbe  kutoka Mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha. 

Image

Katika mazungumzo  hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba, jijini Dodoma viongozi hao wamejadili kuhusu nafasi ya Mahakama  ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika kusimamia na kulinda Haki za Binadamu na Watu wa Afrika. 

Image

Waziri Kabudi amesema yapo maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa zaidi katika Mahakama ili kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo ambapo pia wamejadili changamoto zinazoikabili sekta ya Mahakama ambapo wamekubaliana kuendeleza majadiliano kwa ajili ya kuzifanyia kazi changamoto hizo ili kuiwezesha Mahakama kutimiza majukumu yake ambayo imepewa chini ya Mkataba wa kuanzishwa kwa  Mahakama hiyo.

Image