Skip to main content

USALAMA BARABARANI NI NGAO YA MAISHA KILA MMOJA ANA WAJIBU WA KUFUATA SHERIA – KOPLO REHEMA MAKALA

Submitted by admin on 2 March 2025

Jeshi la Polisi laendelea Kutoa Elimu ya Kisheria juu ya Usalama Barabarani. 

Elimu ya kisheria inaendelea kutolewa na Koplo Rehema Makala, askari wa usalama barabarani, ambaye ameendelea kutekeleza jukumu lake la kutoa maarifa kwa wananchi kwa lengo la kuimarisha usalama barabarani.  

Kupitia juhudi za Jeshi la polisi, Koplo Rehema anahamasisha wananchi kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara. 

Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa  Wizara ya Katiba na sheria kwa kushirikiana  Jeshi la Polisi Tanzania kusaidia jamii kuwa na uelewa mpana kuhusu haki na wajibu wao barabarani.   #sisinitanzania #mslac #katibanasheria #ssh #ccm #kaziiendelee #matokeochanya #nchiyangukwanza #habari #news