Skip to main content

"Utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia una malengo makuu manne ambayo ni ....

Submitted by admin on 20 January 2025

Moja Kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya haki, mifumo ya kisheria iliyopo, haki za binadamu na haki za makundi maalumu, mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na masuala ya upatikanaji haki kwa ujumla; 

Pili; kulinda na kukuza haki kupitia mfumo wa msaada wa kisheria; 

Tatu; kuboresha upatikanaji wa haki kwa wasio na uwezo wa kumudu gharama hususani wanawake, watoto, wazee watu wenye ulemavu na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu na hatarishi na; 

Nne; kuimarisha amani na utulivu na kuchangia katika maendeleo ya watu na ustawi wa jamii.