Skip to main content

WAKATI MWINGINE HAKUNA MIGOGORO BALI NI UKOSEFU WA UELEWA WA SHERIA. - DKT. SCHOLASTICA MALITY

Submitted by admin on 4 April 2025

“Mambo mengi yanatatuliwa kwa kupata elimu. Wakati mwingine hakuna migogoro bali ni ukosefu wa uelewa wa sheria. Kwa hiyo, nampongeza Mama (Rais Samia Suluhu Hassan) kwa kuja na wazo hili zuri mno. Maono yake yanaleta msaada mkubwa sana kwa wananchi.”

Hayo yamesemwa na Dk. Scolastica Maliti, akisisitiza umuhimu wa elimu ya kisheria kwa jamii katika kupunguza migogoro na kuimarisha haki kwa wote. Dk. Maliti ameweka wazi kuwa changamoto nyingi zinazowakabili wananchi zinaweza kutatuliwa kwa njia ya maarifa sahihi juu ya sheria na haki zao za msingi.

Amesisitiza kuwa jitihada zinazofanywa kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (MSLAC) ni miongoni mwa hatua bora kabisa zilizowahi kufikiwa nchini kwa lengo la kusogeza huduma za kisheria kwa wananchi wa kawaida. Kupitia kampeni hii, wananchi wengi wamepata fursa ya kujifunza, kuuliza maswali, na kupata msaada wa kisheria bila malipo – jambo ambalo limeleta mwamko mpya wa haki, utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani, na kuimarika kwa mshikamano wa kijamii.

Kwa mujibu wa Dk. Maliti, maono ya Rais Samia siyo tu kwamba ni ya kimapinduzi, bali pia yanaakisi uongozi wenye huruma na uzalendo wa kweli kwa wananchi.