Skip to main content

Wakazi wa Mkoa wa Arusha wameitikia kwa wingi wito wa kushiriki katika kampeni ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan

Submitted by admin on 1 March 2025

Ilizinduliwa rasmi tarehe 1 Machi 2025 mkoani Arusha. Kampeni hii imelenga kuwasaidia wananchi kutatua migogoro yao mbalimbali na kutoa elimu kuhusu msaada wa kisheria.

Image

Kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, wakazi wa Arusha wameonyesha mwitikio mkubwa kwa kuhudhuria kliniki za kisheria zilizowekwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa. Wananchi wengi wameripoti kupata uelewa wa namna ya kushughulikia changamoto zao za kisheria, ikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, na masuala ya kifamilia.

Image

Viongozi hao wamewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kuendelea kushiriki kikamilifu katika kampeni hii. Aidha, wamewasihi waendelee kutumia fursa hii muhimu ili kuhakikisha haki inapatikana na amani inadumishwa katika jamii. Kampeni hii inatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi wa Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.Image #katibanasheria #mslac #SSH #kaziiendelee #sisinitanzania #matokeochanya #nchiyangukwanza #tiktoktanzania #tiktokviral #tiktok #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #news