Skip to main content

Wananchi Mnaida Wanufaika na Elimu na Huduma za Kisheria Kupitia Kampeni ya Mama Samia

Submitted by admin on 31 January 2025

Image

Katika kijiji cha Mnaida, kata ya Tangazo, Halmashauri ya Mtwara DC, wananchi wameendelea kunufaika na elimu ya sheria pamoja na huduma za msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign. Kampeni hii inalenga kuwawezesha wananchi kuelewa haki zao za kisheria na kupata usaidizi wa kisheria bila gharama, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote. Huduma hii imepokelewa kwa mwitikio mkubwa, huku wakazi wa eneo hilo wakielezea manufaa yake katika kuboresha maisha yao ya kijamii na kijinai.

Image