Skip to main content

"WANANCHI TUMIENI FURSA HII YA MSAADA WA KISHERIA" – MHE. ANJELINA MABULA

Submitted by admin on 18 February 2025

Mbunge wa Ilemela, Mhe. Anjelina Mabula, amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Mwanza, hususan wilaya ya Ilemela, kutumia fursa ya msaada wa kisheria unaotolewa kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC).

"Huduma hii ni muhimu kwa wananchi, hasa wale waliokuwa wakikosa haki zao kutokana na changamoto za kisheria. Nawahimiza wananchi wote kuchangamkia fursa hii ili kupata uelewa na utatuzi wa changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili," alisema Mhe. Mabula.

Aliongeza kuwa msaada wa kisheria unahusisha masuala ya ardhi, ndoa, mirathi, ajira, unyanyasaji wa kijinsia, na haki za watoto, jambo linalosaidia kupunguza migogoro katika jamii.

Kampeni hii inaendelea kufanikisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha haki inapatikana kwa wote bila ubaguzi wa kiuchumi au kijinsia.