Katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia uliofanyika mkoani Tanga, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amemsikiliza Elisha John, mchezaji wa mpira wa miguu mstaafu, aliyewasilisha mgogoro wake unaohusiana na masuala ya haki na ustawi wa maisha yake baada ya kustaafu.
Elisha John ameeleza hadharani changamoto zake mbele ya Waziri na umati wa wananchi, akisisitiza umuhimu wa wachezaji wastaafu kupata haki zao, hasa kuhusu mafao, mikataba ya zamani, na utambuzi wa mchango wao katika taifa.
Mhe. Ndumbaro ametoa maelekezo ya awali na kuahidi kuwa serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria itafuatilia suala hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha haki inapatikana bila upendeleo.