Kwa mda ambao mmefanya kampeni hii nimefurahi kupata taarifa kuwa mmeshakwenda kwenye halmshauri 42, kata 452 na Vijiji 1348 mmevifikia na toka mmeanza hii kampeni watu wengi mmeweza kuwafikia""Watu 415,597 mmewasikiliza na hapa nataka kutofautiana na Mhe. Waziri wa Maendeleo ya Jamii (Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima)...katika idadi ya watu hiyo mliyowafikia kupitia kampeni hii, Wanaume ni 216,000 wakati Wanawake ni 199,000..."Kwahiyo Wanaume wameanza kujitokeza kwa wingi kulingana na namba hizi ambazo tumekwisha kuziona na bila shaka wataendelea kuja kwasababu mwanzo huko nyuma pengine ilikuwa mushikeli kidogo kwa Mwanaume kulalamika unakufa na tai shingoni, lakini baada ya kampeni hii tumeona wanaume wengi wameendelea kujitokeza na bila shaka wataendelea kujitokeza kwa wingi" Mhe. Dkt. Dotto Biteko (Mb) (Mgeni Rasmi) Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Nchini Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, leo tarehe 26 Mei, 2024 mkoani Njombe.