Skip to main content

AOMBA SERIKALI KUPELEKA KAMPENI YA MSLAC VIJIJINI AMBAPO KUNA UELEWA MDOGO WA ELIMU YA SHERIA

Submitted by admin on 7 August 2024

Lusian Mwanitu, mkazi wa mkoani Dodoma, ameomba serikali kuongeza nguvu kwenye kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ili iweze kuwafikia watu wengi zaidi, hususan wale waliopo vijijini. Mwanitu amepongeza juhudi za kampeni hiyo, akisema kuwa ni taasisi mpya na yenye manufaa makubwa kwa Watanzania. 

"Serikali inapaswa kuongeza rasilimali na nguvu kwenye kampeni hii ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, kwani imeonyesha uwezo mkubwa wa kuwasaidia wananchi, hasa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za kisheria," alisema Mwanitu. 

Aliongeza kuwa kampeni hii inatoa msaada muhimu kwa watu wanaokumbana na matatizo mbalimbali ya kisheria, na kwamba ni muhimu kuhakikisha huduma hizi zinawafikia watu wengi zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uelewa wa haki za kisheria ni mdogo. Mwanitu anaamini kuwa kwa kuimarisha kampeni hii, serikali itakuwa inachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha wanapata haki na usawa mbele ya sheria