Skip to main content

Elimu ya Haki: Watoa Huduma wa Kisheria Wafundisha Wanafunzi Kuhusu Ukatili wa Kijinsia

Submitted by admin on 13 February 2025

Halmashauri ya Mtwara Dc, Kata ya Mayanga, Kijiji cha Msijute Katika jitihada za kuimarisha elimu ya haki na usalama miongoni mwa vijana, watoa huduma za msaada wa kisheria walitembelea shule ya msingi Msijute. Ziara hii ililenga kuwafundisha wanafunzi kuhusu hatari na athari za ukatili wa kijinsia, huku wakiwasaidia kujua haki zao na njia za kujikinga

Image

Hatua hii inachukuliwa kama juhudi muhimu za kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa usalama wa watoto na ulinzi dhidi ya aina zote za ukatili. Serikali pamoja na mashirika husika wanaendelea kuhimiza elimu ya haki ili kuhakikisha ustawi na maendeleo ya kijamii.

Image Kaziiendelee