Kwa kuzingatia Katiba ya Tanzania na Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Mslac Inatoa msaada wa kisheria bure kwa watu wanaokumbwa na migogoro ya ndoa, ikiwa ni pamoja na ushauri kuhusu haki zao ndani ya ndoa, usuluhishi wa migogoro, na masuala ya talaka na malezi ya watoto.