Mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa Huduma za Msaada wa Kisheria katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid Campaign)
Kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Kigoma yanaendelea katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Kampeni ya MSLAC inaanza rasmi tarehe 24/1/2025 katika mikoa 6 ukiwemo mkoa wa Kigoma na wilaya zake zote.