Hadithi hii inamgusa Bwana Steven Mgolwa, mjumbe wa mtaa aliyejitokeza kusaidia watoto wawili ambao walitelekezwa baada ya mama yao kulazimika kuondoka kutafuta maisha. Mtoto mmoja ana miaka 14 na anaishi na changamoto ya selimundu, na mdogo wake ana miaka 5.
Kupitia ushirikiano kati ya mjumbe, majirani na ustawi wa jamii, tulifanikiwa kumfikia mama mzazi na baada ya miezi 8 akarudi nyumbani kuendelea kulea watoto wake. Hata hivyo, mama huyu bado anakabiliana na maumivu ya maisha, historia ya malezi magumu, kuachwa mara kadhaa na kukosa nafasi ya kusoma au kupata msaada wa kudumu.
Hii ni safari ya kugusa moyo inayokumbusha umuhimu wa kushikamana, kuchukua hatua na kusaidia familia zinazopitia changamoto kubwa kimwili, kijamii na kisaikolojia.