Skip to main content

MSLAC Yatoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa Wananchi wa Mabogini, Kilimanjaro

Submitted by admin on 7 February 2025

Image

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (MSLAC) inaendelea na shughuli zake za kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi katika kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Wananchi wamepata mafunzo juu ya masuala ya ardhi, mirathi, ndoa, migogoro ya kifamilia, ajira, na mbinu za utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kama usuluhishi na maridhiano.

Kampeni hii inalenga kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria na kuwahamasisha kutumia njia sahihi za kutatua migogoro ili kujenga jamii yenye usalama na mshikamano. Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha haki inapatikana kwa wote.

Image

#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango @DBiteko

@katibanasheria_ @profkabudipjam @victoriacharlz

@tanganyikalawsociety @BMWABUKU