Skip to main content

MZEE, SISI TUMETUMWA KUWATETEA WANYONGE NA KUPAMBANIA HAKI ZAO – MSLAC

Submitted by admin on 15 October 2025

Mzee Fanuel Julius Gota, mkazi wa mkoa wa Kigoma, amepata haki yake kupitia msaada wa kisheria uliotolewa na watoa huduma wa MSLAC.

Baada ya kupitia changamoto ya mgogoro wa ardhi dhidi ya mwenyekiti wa kijiji, Mzee Gota alipokea msaada wa kisheria bila malipo kutoka kwa timu ya MSLAC waliokuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanyonge.

Watoa huduma hao walisisitiza dhamira yao kwa maneno haya: “Mzee, sisi tumetumwa kuwatetea wanyonge na kupambania haki zao – MSLAC.”

Video hii inaonyesha safari ya haki ya Mzee Gota — kutoka kwenye mateso ya muda mrefu hadi kupatikana kwa suluhu kupitia msaada wa kisheria. Ni ushuhuda wa kweli wa namna huduma za MSLAC zinavyogusa maisha ya wananchi wa hali ya chini.

🎯 MSLAC – Kutetea haki, kulinda utu, na kujenga jamii yenye usawa.

#MSLAC #HakiKwaWote #MsaadaWaKisheria #Kigoma #HakiZaBinadamu #LegalAid #MSLACKigoma